Ijumaa 17 Julai 2026 - 12:00
Hafla ya "Imamu wa Mashahidi" Yafanyika huko Al-Hermel, Lebanon kwa Kumuenzi Imam Khamenei

Hawza / Harakati ya Hizbullah ya Lebanon pamoja na Jumuiya ya Vituo vya Utamaduni vya Imam Khomeini (qs) zimeandaa hafla iliyopewa jina la "Imamu wa Mashahidi" kwa ajili ya kumuenzi Kiongozi Shahidi, Imam Sayyid Ali Khamenei (qs), pamoja na wenzake mashahidi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah ya Lebanon kwa kushirikiana na Jumuiya ya Vituo vya Utamaduni vya Imam Khomeini (qs), iliandaa hafla iliyopewa jina la "Imamu wa Mashahidi" kwa lengo la kumuenzi Kiongozi wa Kimataifa Shahidi, Ayatullah al-Udhma Imam Sayyid Ali Khamenei (qs), pamoja na wenzake waliopata daraja la ushahidi.

Hafla hiyo ilifanyika katika eneo la Majma' Sayyid al-Shuhadaa (as) iliyopo katika mji wa Al-Qasr, eneo la Al-Hermel, kwa kuhudhuriwa na wanazuoni wa dini, familia tukufu za mashahidi, idadi ya viongozi na watu wa eneo hilo pamoja na wakazi wa mkoa huo.

Katika hafla hiyo, Sheikh Hussein Zain al-Din alitoa hotuba ambapo alichambua nafasi ya kimkakati ya Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kujenga kwa uthabiti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuuongoza Umma wa Kiislamu kuelekea uhuru.

Katika sehemu ya hotuba yake alisema: "Ndiyo maana Donald Trump, Rais wa Marekani, alimuua shahidi akiwa katika handaki la jihadi, hali ya kuwa amefunga saumu na alikuwa akishughulika na usomaji wa Qur'ani Tukufu."

Katika sehemu nyingine ya hafla hiyo, ilioneshwa filamu ya kumbukumbu kuhusu mwenendo wa maisha ya Kiongozi huyo Shahidi. Mwishoni mwa hafla hiyo, kulifanyika kikao cha kuomboleza na kusomwa tenzi za maombolezo kwa sauti ya Sheikh Hassan al-Baba.

Hafla ya "Imamu wa Mashahidi" Yafanyika huko Al-Hermel, Lebanon kwa Kumuenzi Imam Khamenei

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha